DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amewataka watanzania kuwa wepesi katika kuchangia katika matibabu ya magonjwa kuliko sherehe na misiba.
Akizungumza wakati wa kuchangia taasisi ya msanii, Joseph Haule kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Naibu Waziri wa Afya Dk Mollel amesema kuwa watanzania ni rahisi kuchangia harusi kuliko unapokuwa na ugonjwa.
“Ingekuwa tunachangia harusi tungepata pesa nyingi kuliko tunapochangia ugonjwa au kifo, kuna magonjwa yanahitaji pesa nyingi za matibatu ndugu peke yake hawatoshi wanahitaji msaada wa dawa pamoja na matibatu.”amesema
Dk Mollel amesema Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa amechangia kiasi cha Sh million 10, pamoja na kuchangia bima ya afya kwa wagonjwa 1000 watakaohudumiwa kwenye Profesa Jay Foundation.
Aidha viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Vyama vya Siasa waliwasilisha michango yao katika uzinduzi wa taasisi hiyo.