Dk Mpango akabidhi hatimiliki za kimila Makete

NJOMBE: Makamu wa Rais Dk. Philip Isdori Mpango amekabithi Hati ya Hakimiliki za Kimila kwa wananchi wa Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe.
 
Dk. Mpango amekabidhi hati saba za mfano kati ya Hatimiliki za Kimila 6,883 zilizoandaliwa tarehe 27 Oktoba 2023 katika halfa iliyofanyika Kijiji cha Tandala wilayani humo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoa wa Njombe.
Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda amesema, utolewaji Hati za Kimila wilayani Makete unafuatia uwezeshwaji uandaaji mipango ya matumizi bora ya ardhi uliofanywa na wizara yake kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi katika vijiji.
 
Kwa mujibu wa Pinda Mkoa wa Njombe una jumla ya vijiji 323 ambapo vijiji 264 kati ya hivyo tayari vimewezeshwa kuandaliwa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
 
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe amesema kuwa, upatikanaji wa Hatimiliki hizo ni jitihada za Wilaya kukuza zao la ngano àlilolieleza kuwa linazalishwa kwa wingi katika Wilaya hiyo.
 
Ugawaji wa Hatimiliki hizo unafuatia kazi iliyofanywa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi iliyowezesha uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 64 katika wilaya ya Makete na kutoa jumla ya Hatimiliki za Kimila 6,889.

Habari Zifananazo

Back to top button