Dk Mpango ataka wanaoishi Marekani wafuate sheria

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango, amewaasa Watanzania waishio Marekani na nchi nyingine duniani, kuishi kwa kufuata sheria za nchi hizo na kujiepusha na vitendo vya kihalifu vitakavyoharibu taswira ya Tanzania.

Dk Mpango ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania waishio jijini New York, Marekani, katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania jijini New York.

Pia Makamu wa Rais aliwaambia diaspora hao kuwa, serikali inathamini na kutambua mchango wao katika kuleta maedeleo nchini na kwamba itaendelea kuunga mkono jitihada hizo.

Amewaasa kuendelea kuitangaza vyema Tanzania, kuvutia wawekezaji pamoja na kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini.

“jitahidini kutafuta masoko ya bidhaa na malighafi za Tanzania katika nchi mnazoishi kwa manufaa ya Watanzania walio wengi,” alisema.

Aliwashauri kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa kuanzisha vituo vya kujifunzia lugha ya hiyo katika maeneo waliyopo.

“Suala la utangazaji wa lugha ya Kiswahili linapaswa kwenda sambamba na kutangaza utamaduni wa taifa la Tanzania, pamoja na vivutio vizuri vilivyopo,” Dk Mpango alisema. upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amesema Wizara ya Mambo ya Nje ipo kwenye mchakato wa kutengeneza sera ya mambo ya nje, ambayo inatambua mchango wa diaspora.

Amesema Wizara itazindua kanzu data, ambayo itawezesha wanadiaspora kutambulika popote walipo duniani.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x