Dk Mpango atoa pole vifo vya watu 25 Arusha

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango ameungana na Rais Samia kutoa pole kwa wote walioguswa na vifo vya watu 25 waliokufa katika ajali ya magari manne iliyotokea jana eneo la Ngaramtoni Kibaoni Arusha.

Ninaungana na Mheshimiwa Rais katika kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne katika eneo la Ngaramtoni Kibaoni Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha tarehe 24 Februari 2024.” Ameandika Dk Mpango kupitia wa X.

Dk Mpango ametoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani sambamba na kuendesha vyombo vya moto vilivyokaguliwa.

“Mwenyezi Mungu azipokee roho za marehemu na kuziweka mahala pema peponi. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu awajaalie uponyaji majeruhi wote wa ajali hiyo”. Ameongeza Dk Mpango.

Habari Zifananazo

Back to top button