Dk Mpango awasili Marekani

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango leo amewasili New York Marekani kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa (UNGA78).

Dk Mpango ataongoza pia Ujumbe wa Tanzania katika mikutano mbalimbali inayohusu mazingira, uchumi, afya, maji, demokrasia na malengo ya maendeleo endelevu.

Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Mataifa York Septemba 21, 2023.

Imeandaliwa Na Rahimu Fadhili

Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi

Una maoni usisite kutuandikia

Habari Zifananazo

Back to top button