Dk Mpango aweka jiwe la msingi mradi wa maji Mowe

TANGA: Makamu wa Rais Dk Philip Mpango akiweka jiwe la msingi katika mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Tanga kupitia Hatifungani katika eneo la Mtambo wa kutibu na kuzalisha maji wa Mowe uliopo eneo la Pande, mkoani Tanga.

Makamu wa Rais akishiriki katika ratiba hiyo amepokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Mradi huo umelenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi ya uhakika katika maeneo ya Jiji la Tanga, miji ya Muheza, Pangani na Mkinga wenye thamani ya Sh bilioni 53.

12 zitakazopatikana kupitia uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya Tanga UWASA na unatarajiwa kutekeleza ndani ya mwaka mmoja kuanzia Aprili, 2024.

Habari Zifananazo

Back to top button