Dk Mpango: Fundisheni watoto uzalendo

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango ameelekeza kwa wazazi kulea watoto wao vyema, kuwafundisha uzalendo na kufanya kazi kwa bidii ili kuwa raia wema ikibidi baadaye wawe viongozi waadilifu.

Dk Mpango ametoa maelekezo hayo alipoungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo Desemba 25, 2023.

Kiongozi huyo amesema wakati dunia ikiendelea kusherehekea Sikukuu ya Krismas, Watanzania wanapaswa kujitafakari na kuachana na tabia za kutupa watoto pamoja na utoaji wa mimba na kupinga aina zote za ukatili.

Akitoa salamu za Krismasi, Makamu wa Rais amewasihi Watanzania kusheherekea sikukuu kwa amani na utulivu pamoja na kujitoa kusaidia wale wasio na uwezo wakiwemo yatima.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button