Dk Mpango: Nilikwenda nje kufanya shughuli maalum

DODOMA: MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amewaasa watanzania kutumia vema mitandao ya kijamii. Amesema matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Dk Mpango amezungumza hayo alipoungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo tarehe 10 Desemba 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.
“Asanteni sana kwa kuniombea. Yamesemwa mengi si ndio? Na wengine wanasema mimi ni mzuka” amesema Dk Mpango
Amesema kwa takribani mwezi mmoja ambao hakuwa masikioni wala machoni mwa wengi ni kwa sababu alikuwa nje ya nchi kwaajili ya shughuli maalumu.
“Wengine wanasema mzee amakata moto. Bado kabisa, kazi ambayo Mungu amenituma kufanya sijaimaliza.” Amesema Dk Mpango.

Habari Zifananazo

Back to top button