SERIKALI inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha Shilingi trilioni 43. 29 kwa mwaka wa fedha 2023/24, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.
4 ya bajeti inayotekelezwa mwaka huu wa fedha, 2022/23.
Bajeti inayotekelezwa kwa mwaka huu wa fedha, 2022/23 ni Shilingi trilioni 41.48.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba bungeni leo Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya Mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya Serikali na mapendekezo ya Mpango Wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2023/24.
“Ongezeko hili limezingatia mwenendo halisi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani na jitahada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kuongeza mapato.
“Aidha, ongezeko hilo limezingatia mahitaji yasiyoepukika (first charge expenditure) kama vile mikataba ya kugharamia miradi mbalimbali, deni la Serikali na mishahara ya watumishi wa umma,” amesema Waziri Mwigulu.
Akifafanua zaidi, Dk Mwigulu amesema, katika mwaka wa fedha 2023/24, mapato ya ndani yanakadiriwa kuwa Shilingi trilioni 31.03 sawa na asilimia 71.7 ya bajeti yote.
Akieleza zaidi, amesema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Shilingi trilioni 4.5, sawa na asilimia 10.9 ya bajeti.
Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 5.64 kutoka soko la ndani ambazo zinajumuisha Shilingi trilioni 3.54 kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na Shilingi trilioni 2.096 kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.
“Vile vile, mikopo ya masharti ya kibiashara kutoka nje inatarajiwa kuwa Shilingi bilioni 2,110.
6 [Sh trilioni 2.11].
“Mheshimiwa Spika, baadhi ya mikakati itakayotumika katika kufikia lengo la makusanyo ya mapato ya ndani ni pamoja na kuendelea: kuwatengea wafanyabiashara na watoa huduma wadogo maeneo maalum kwa lengo la kukuza biashara zao; kutambua na kusajili kampuni za kimataifa,” amelieleza Bunge ambalo muda wote huu lilikuwa limeketi kama kamati.
Baada ya wasilisho la Kamati ya Bunge ya Bajeti, Spika Dk Tulia Ackson ameliahirisha Bunge ili wabunge wapate fursa ya kupitia hotuba hizo kabla ya kuanza kujadili