Dk Mwinyi afanya uteuzi Wizara ya Maendeleo ya Jamii

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amemteua Salum Khamis Rashid kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 18, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu ya Zanzibar, Zena Ahmed Said imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza rasmi leo.

Kabla ya uteuzi huo, kiongozi huyo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Utafiti, Tume ya Mipango Zanzibar.

Advertisement

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *