Dk Mwinyi aguswa kifo cha Jecha

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha.

Taarifa iliyotolewa leo Julai 18, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Charles Hilary imeeleza kuwa Rais Mwinyi ameisihi familia ya Jecha kuwa na subira katika kipindi hiki cha kuondokewa mpendwa wao.

“Sisi sote wa Mungu na kwake tutarejea.”amesema Rais Mwinyi.

Advertisement

Jecha amefariki leo akiwa katika Hospitali ya Lugalo Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Maziko yanatarajiwa kufanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja Visiwani Zanzibar.

1 comments

Comments are closed.

/* */