Dk Mwinyi amuwakilisha Samia Jamhuri Day

KENYA; Nairobi. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kenya.

Akitoa salamu kwenye sherehe hizo jijini Nairobi, leo Desemba 12, 2023, Dk Mwinyi alimshukuru Rais wa Kenya, Dk William Ruto kuwaalika katika sherehe hizo.
“Naatoa shukran kwa Mhe. Dk. William Samoei Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya, kwa kutualika kushiriki kwenye siku hii muhimu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Kenya, maarufu kama Jamhuri Day.

“Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania alitamani sana kuhudhuria kwenye sherehe hizi; hata hivyo, kutokana na majukumu mengine ya kitaifa yanayomkabili, ameshindwa kujumuika nanyi.
“Kama mnavyofahamu, Desemba 2, 2023 baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa nchi yetu yalikumbwa na athari kubwa za mafuriko.

Hivyo, Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa sasa anaongoza jitihada za serikali za kushughulikia changamoto. Hii ndiyo sababu amenituma nije kumwakilisha.

Habari Zifananazo

Back to top button