Dk Mwinyi ashiriki ibada ya mazishi kiongozi ACT

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kumsalia marehemu Habib Ali Mohamed.

Dk Mwinyi amejumuika katika ibada hiyo katika Msikiti wa Masjid Zinjibar uliopo Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Marehemu Habib Ali Mohammed amefariki dunia, leo Machi 03, 2023, Jijini Dar es Salaam katika hospitali ya SAIFEE alipokuwa akipatiwa matibabu.

Habib Ali Mohammed alikuwa mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe lililopoa kisiwani Pemba kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Habari Zifananazo

Back to top button