Dk Mwinyi asifu matunda, mbogamboga kukuza uchumi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema kilimo cha matunda, mbogamboga na viungo kina mchango mkubwa kwenye maendeleo ya uchumi Zanzibar kwa kuwa ni chanzo cha ajira na kipato kwa Wazanzi bari wengi.

Dk Mwinyi alisema kilimo cha mazao ya bustani Zanzibar kimekuwa kikikua katika kipindi cha muongo uliopita baada ya ujio wa taasisi ya Chama cha Waku lima wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA) visiwani humo.

Alisema hayo Zanzibar jana wakati wa uzinduzi wa kituo cha maarifa cha mazao hayo. Dk Mwinyi alisema katika mwaka 2021/2022, uzalishaji wa mazao hayo Zanzibar ulifikia tani 148,000  kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 68.2 katika kip indi cha tangu mwaka 2012.

“Ongezeko la uzalishaji limepelekea kupungua kwa utegemezi ambapo uagizaji wa matunda na mbogam boga kutoka nje ya nchi umepungua kutoka asilimia 80 mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 26 mwaka 2021,”

alisema. Dk Mwinyi alisema ongezeko hili la uzalishaji limewezesha kutengeneza pato la mkulima wa mazao ya bustani kwani kwa sasa nchi inaweza kuzalisha na kuuza mazao yake ndani.

Alisema kilimo hicho pia ni mhimili wa lishe na afya bora kwa wananchi kwa kuwa utumiaji wa mazao ya mbogamboga, matunda na viungo humpa mlaji virutubisho muhimu kwa ajili ya kujenga na kutunza miili na kuwezesha awe na afya njema.

Alisema inakadiriwa asil imia zaidi ya 90 ya mazao na bidhaa zote za matunda, mbogamboga na viungo zinazozalishwa Zanzibar zinauzwa na kutumiwa na wananchi wa visiwani humo na watalii.

“Kwa idadi yetu ya watu karibu milioni 1.9, Zanzibar inahitaji tani 276,000 za mbogamboga na matunda kwa mwaka ili kukidhi mahitaji na kuwezesha kila Mzanzibari ale kilo 146 za mazao hayo kwa mwaka,” alisema.

Aliishukuru Taha kwa kuendeleza uchumi wa Zanzibar. Alisema serikali inatambua na kuthamini mchango wao kwenye ajira kwa wanawake, vijana, ku boresha lishe na kuongeza pato la mkulima.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x