Dk Mwinyi ataka takwimu za sensa kufanyiwa kazi

SERIKALI ya Zanzibar imesema ina jukumu la kuzifanyia kazi takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ili kujipanga na utekelezaji wa mipango ya maendeleo, kiuchumi na kijamii.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alisema hayo Ikulu, Zanzibar alipopokea ripoti ya Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka jana.

Dk Mwinyi alisema sensa hiyo imetoa mambo mengi ambayo lazima yafanyiwe kazi kabla ya kukamilika kwa mpango wa Maendeleo 2025-2030 kuelekea mwisho wa Dira ya Maendeleo ambapo mwaka 2030 alielezea Zanzibar itakadiriwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu.

Advertisement

Alisema ripoti hiyo na nyingine zitakazofuata lazima zitafutiwe namna nzuri ya kufanyiwa kazi kwa undani ili serikali ijipange katika masuala mazima ya maendeleo ya nchi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah alimuahidi Dk Mwinyi na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba kamati yao ya ushauri wa sensa kitaifa itajitahidi kuendeleza sehemu ndogo iliyobaki ili kukamilisha kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *