Dk Mwinyi ateua Mkurugenzi Mkuu ZBC

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein mwinyi amemteua Ramadhan Bukini kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 25, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu ya Zanzibar, Zena Ahmed Said imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza leo.

Aidha, kabla ya uteuzi huo Ramadhan Bukini alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Plus Networks Ltd.

Habari Zifananazo

Back to top button