ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amemteua, Joseph Abdalla Meza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza leo Machi 17, 2024.