Dk Mwinyi ateua Mwenyekiti,  Wajumbe Tume ya Uchaguzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi ameteua Mwenyekiti na wajumbe sita wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Zena Said leo Agosti 24, 2023 imesema Rais Mwinyi amemteua Jaji George Joseph Kazi kuwa Mwenyekiti wa tume hiyo.

Wajumbe walioteuliwa ni Jaji Aziza Iddi Suwedi, Idrisa Haji Jecha, Juma Haji Ussi, Halima Mohammed Said, Ayoub Bakari Hamad na Awadh Ali Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wao unaanza leo na wataapishwa Jumatatu Agosti 28, 2023.

 

Habari Zifananazo

Back to top button