ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amemteua Juma Chum Juma kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar.
Taarifa ilitolewa leo Mei 31, 2024 na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Juma Yakuti Juma imeeleza kuwa Rais Dk Mwinyi pia amemteua Abdallah Ramadhani Nyonje kuwa Mrajis wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar.
Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeenza leo Mei 31, 2024.
Kabla ya uteuzi huo, Juma Chum Juma alikuwa Mrajisi wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar.