Dk Mwinyi awafariji kifo cha aliyeshiriki Muungano

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapimduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu na jamaa kufuatia kifo cha Bi Khadija Abbas Rashid kilichotokea Agosti 22, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hillary, Rais Mwinyi ameiomba familia ya marehemu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Dk Mwinyi alimtembelea marehemu na kumjulia hali nyumbani kwake wakati alipokuwa anaumwa wiki mbili zilizopita.

Advertisement

Marehemu Bi Khadija ni miongoni mwa wanawake walioshiriki katika tukio la kihistoria lililofanyika Aprili 26, 1964 la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kuashiria muungano wa nchi mbili.

Tukio hilo la kihistoria lilifanywa na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Amani Abeid Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *