Dk Mwinyi azindua mfumo wa kielektroniki uwekezaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara katika uwekezaji nchini.
Dk Mwinyi amesema hayo leo Machi 10, 2023 wakati akizindua Muongozo wa Uwekezaji na Mfumo wa Kieletroniki wa Uwekezaji (ZIPA) wenye madhumuni ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wawekezaji ikiwemo usajili na upatikanaji wa cheti cha uwekezaji wenye jina la”ZANZIBAR INVESTMENT ELECTRONIC WINDOW” (ZieW).
Dk Mwinyi amesema kukuza uwekezaji ni moja ya malengo makuu ya Serikali na kuleta Maendeleo.