Dk Mwinyi kuiongoza familia ya Mwinyi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kabla ya kifo cha baba yake hayati Ali Hassan Mwinyi alimpa jukumu la kuiongoza familia.

Akimzungumzia baba yake katika ya khitma iliyofanyika leo Zanzibar kumuombea kiongozi huyo, Dk Mwinyi amesema alipewa jukumu hilo na kulipokea.

“Nakuagiza wewe utakuwa msaidizi wa familia, sio kwa sababu wewe ndio mkubwa, wapo wakubwa zako lakini kwa sababu ya wadhifa wako, nawaweka ndugu zako hawa chini ya muongozo wako, nikalipokea Mwenyezi Mungu anisaidie,” amesema Dk Mwinyi.

Dk Mwinyi amesema Rais Samia ndiye ameiwezesha khitma hiyo kwani kabla ya familia haijapanga lini na wapi itafanyika Rais Samia aliwataka wanafamilia wamruhusu aifanye yeye.

“Aigharamie yeye na tukakubaliana tuifanye hapa na Alhamdullilah mmekuja kwa wingi tumemuombea dua mzee wetu na imewezeshwa na Rais wetu, hivyo tunasema tunamshukuru sana, mwenyezi Mungu amlipe kila la Kheri”, ameongeza Dk Mwinyi.

Habari Zifananazo

Back to top button