Dk Mwinyi: Tumejipanga kuimarisha maadili, haki za binadamu

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema serikali imejipanga vema kuimarisha maadili, haki za binadamu na misingi ya utawala wa bora nchini.

Rais Mwinyi amesema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi leo Desemba 19, 2023.

Amesesma mafanikio ya kimaendeleo yanayopatikana nchini yanachangiwa na uimara na umadhubuti wa taasisi zinazosimamia utawala bora akitolea mfano ZAECA, CAG,Tume ya Maadili,Tume ya Haki za Binadamu, Idara ya Utawala Bora, DPP na Mahakama.

Advertisement

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma kwa mujibu wa sheria ya Maadili kuhusu katazo la matumizi mabaya ya madaraka na cheo kwa manufaa binafsi, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria wale watakaobainika kuwa na makosa .

Pia amewataka viongozi mbalimbali wahakikishe wanajaza Fomu za Tamko la Rasimali na Madeni na kuzirejesha katika Ofisi za Tume ya Maadili kwa wakati uliowekwa kwa mujibu wa Sheria na si zaidi ya Desemba 31 mwaka huu , hatua zitachukuliwa kwa viongozi watakaochelewa kurejesha fomu hizo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *