Dk Nchimbi aonya wanaotanguliza maslahi binafsi

KAGERA; Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Emmanuel Nchimbi amekemea tabia ya viongozi wanaoendekeza maslahi binafsi na kusema siku zao za uongozi zinahesabika.

Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati wa mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Balozi Dk.Deodorus Kamala aliyefariki Februari 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mazishi hayo yamefanyika Kijiji cha Rwamashonga,Kata ya Bwanjai wilayani Missenyi mkoani Kagera na kueleza kuwa Kamala alitumikia Taifa lake kwa weledi na nguvu zake zote.

Advertisement

Amesema Dk Kamala alikuwa mwanasaikolojia makini, alikataa rushwa na alikuwa mkweli  na kwamba viongozi wa aina hiyo ni wachache duniani.

Amesema Taifa linahitaji viongozi wenye hekima na kulitumikia kwa uadilifu na uaminifu na siyo kwa maslahi yao binafsi, hivyo kwa sasa wanahitajika vionjozi wanaotanguliza maslahi ya umma.

“Wapo viongozi wasiopenda rushwa na wanatumikia Taifa kwa nguvu zao zote katika kuwatetea na kuwalinda kwa sababu wanatimiza wajibu wao, kama inavyotakiwa na wale ambao bado wanasuasua wajitafakari  kuanzia sasa,” amesema.

#MwangwiwaUkarimu #echoesofkindness
#HabarileoUPDATES