ARUSHA: Waziri wa Utamaduni Sanaa Na Michezo, Damas Ndumbaro amefungua rasmi Mashindano ya Kimataifa ya “NCBA Tanzania Open 2023″ya mchezo wa gofu yanayofanyika katika Uwanja wa Kili Golf Jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa shindano hilo amesema kupitia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejipambanua katika kuendeleza michezo pamoja na kutumia michezo kukuza uchumi na ajira kwa watanzania kuku wachezaji watakao ibuka washindi wakijinyakulia zawadi zenye thamani na ubora wa hali ya juu kwenye shindano hilo.
“Michezo ni muhimu na unaweka mwili kwenye afya njema kwa kuwa unaupa mazoezi, naamini washindi watafurahia na kupongezwa” amesema Ndumbaro
“Washiriki wote wameshafika kutoka nchi mbalimbali niwatakie mchezo mzuri na washindi watakaopatikana watajinyakulia zawadi zao zipo tayari.” amesema Gilman Kasiga (Rais Wa chama Cha Mchezo Wa Gofu Tanzania-TGU)
Kwa upande wake mdhamini mkuu wa shindano hilo, Clavar Serumaga amesema amefurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya mchezo wa Gofu na kuahidi kuendelea kushirikiana na Chama cha mchezo wa gofu katika Kukuza mchezo Huo.
Wachezaji Kutoka nchi mbalimbali katika Bara la Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini,Rwanda,Burundi,Ethiopia na Zambia wameshiriki Katika Shindano La NCBA Tanzania Open 2023 Jijini Arusha.