Dk Phumzile kushiriki tamasha la jinsia TGNP
ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Afika Kusini, Dk Phumzile Mlambo Ngcuka anatarajiwa kushiriki katika tamasha la jinsia pamoja na kufikia miaka 30 na Tapo la Kifeminia la mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Mkurugenzi Mtendaji wa TNGP Lilian Liundi amesema hayo Dar es Salaam na kuongeza kuwa tamasha hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1500 litafanyika Novemba 7 hadi 10 mwaka huu.
Amesema tamasha hilo huwashirikisha watu mbalimbali walio mashuhuri na hata viongozi kadha wa kadha, lengo kubwa kujadili mada mbalimbali zenye kujenga na kuimarisha mfumo mzima wa usawa wa jinsia nchini.
Amesema Dk Mlambo ni miongoni mwa washiriki, katika tamasha hilo na ni mtetezi wa kimataifa wa uwezeshaji wa wanawake na wasichana.
Aidha amesema alikuwa Naibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini na Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women global akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo, kiongozi wa juu kabisa wa kisiasa mwanamke katika historia ya Afrika Kusini
Kuhusu tamasha la jinsia amesema ni moja ya jukwaa kubwa la ujenzi wa nguvu na harakati za pamoja.Lengo lake likiwa ni kubadilishana ujuzi, udhoefu na kusherekea maendeleo mbalimbali waliofanya TNGP.
Amesema TNGP imeanzishwa mwaka 1993 hivyo wanatomiza miaka 30 na wamekuwa wakiendesha matamasha tangu mwaka 1996 hadi sasa wamefanya matamasha 14 hivyo la mwaka huu ni la 15 wakitetea mambo mbalimbali.
Amesema katika miaka 30 ya TNGP wanatarajia kuwa na mada mbalimbali za kujadili zenye kushirikisha watu mashuhuri ikiwemo mada ya tapo la ukombozi wa wanawake.
“TNGP imefanya maendeleo mbalimbali kuendeleza usawa wa jinsia nchini, tunaendelea kupambana zaidi mifumo dume tumeona madhara mengi,” amesema na kuongeza kuwa tamasha hilo linatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1500 .