Dk Rose: Wazazi mtumieni Rais Samia kama hamasa

DAR ES SALAAM: IKIWA leo ni siku yam toto wa kike duniani, Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema nafasi ya Rais Samia Suluhu Hassan kama kiongozi, iwe chachu na hamasa kwa jamii kuendelea kuwekeza kielimu kwa mtoto wa kike.

Akizungumza leo Oktoba 11, 2023 Mkurugenzi wa TAMWA Dk Rose ameitaka jamii, hususan wazazi, kuwapa nafasi watoto wa kike na kuendelea kuwekeza katika elimu, kwani sio tu kwamba kundi hilo wana uwezo kielimu lakini pia wana uwezo katika uongozi kama tunavyoona sasa Tanzania ina Rais mwanamke, ambaye ni Dk Samia Suluhu Hassan.

“Nafasi ya Rais Samia Suluhu Hassan kama kiongozi, iwe chachu na hamasa kwa jamii kuendelea kuwekeza kielimu kwa mtoto wa kike,”amesema Rose

Amesema, TAMWA inatambaua changamoto luluki zinazomkabili mtoto wa kike hapa nchini na kuitaka jamii kuwekeza katika elimu ya kumkomboa mtoto wa kike..

“Hivyo tunapoadhimisha siku hii, hatuna budi kuziangazia ili kukumbushana kuwa mapambano yanaendelea ili kumfanya mtoto wa kike kupata haki zake katika jamii.”Amesema Rose

Amesema, TAMWA katika safari yake ya miaka zaidi ya 35 ya kuhamasisha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto wa kike, imekutana na madhila mengi dhidi ya watoto wa kike na miongoni mwa hayo ni ukeketaji, mimba za utotoni, ndoa za utotoni na uminywaji wa haki za kupata elimu kwa watoto wa kike.

“Lakini kadri dunia inavyobadilika ndivyo tunavyoona kuwa ili kuyaondoa hayo yote, basi suluhu la kudumu ni kuwekeza katika elimu. Ndiyo maana kauli mbiu ya mwaka huu inasema: “Wekeza katika haki za watoto wa kike: Uongozi wetu, ustawi wetu’.

“Kauli mbiu hii inajikita katika kuamsha hamasa kwa jamii, asasi za kiraia, serikali na watunga sera kuwekeza katika kuzitambua na kuzitekeleza haki za mtoto wa kike, na pia kutumia nafasi za uongozi kuwastawisha watoto wa kike.”Amesema

Amesema, TAMWA inaipongeza serikali kwa kuwekeza zaidi katika kujenga mabweni na shule za watoto wa kike, kutoa ufadhili wa masomo na kuwapa watoto wa kike kipaumbele katika nafasi za kielimu.

Hata hivyo amesema bado kuna mapengo makubwa katika jamii hasa ya kimtazamo kwamba watoto wa kike hawana umuhimu wa kupata elimu.

“Na hili linakwenda sambamba na mila na tamaduni ambazo zinaamini mtoto wa kike hana haki ya kupata elimu. Hivyo wakati serikali na wadau wengine wakiwekeza katika elimu, wapo wazazi au familia zinazomtupa mtoto wa kike asipate elimu.” Amesema Rose

Aidha, amesema ili kupata suluhisho la changamoto hizo, TAMWA imefanya miradi kadhaa inayolenga kumuinua mtoto wa kike kielimu ikiwemo midahalo kadhaa na watoto wa kike, katika shule za Nambilanje na Likunja, mkoa wa Lindi, shule ya sekondari ya Mugabe, Sinza, Dar es Salaam, nia ni kusikiliza sauti zao na kujua wanachotaka.

“Tunaposikiliza sauti zao, tunajua changamoto wanazopitia na hivyo tunajua wapi pa kuchukua hatua tunapozingatia haja zao, wasichana hawa nao wanaongeza kasi ya kutetea mabadiliko yao katika jamii wanazoishi” Dk Rose

Kwa mfano, katika mdahalo uliofanywa katika shule ya msingi Likunja, watoto wa kike walibainisha kuwa, wazazi huwaambia waandike makosa katika mitihani yao ya kumaliza darasa la saba, ili wasifaulu.

Walimu katika shule hiyo walisema, matukio ya wazazi kuwafundisha watoto wa kike waandike ‘makorokocho’ kwenye mitihani yameongezeka baada ya serikali kujenga zaidi shule za sekondari na hivyo wanafunzi wanaofaulu kuongezeka.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Work At Home
Work At Home
1 month ago

I am making $100 an hour working from home. I never imagined that it was honest to goodness yet my closest companion is earning $16,000 a month by working on a laptop, that was really dumbfounding for me, she prescribed for me to attempt it simply. Everybody must try this for this job now by just using

this site link… http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work At Home
Royal
1 month ago

I’m making $90 an hour working from home. i was greatly surprised at the same time as my neighbour advised me she changed into averaging $100 however I see the way it works now. I experience mass freedom now that I’m my non-public boss. Everybody must try this job now by just using this website……. http://Www.SmartCash1.com

Last edited 1 month ago by Royal
Patrick
Patrick
1 month ago

Google pay 390$ reliably my last paycheck was $55000 working 10 hours out of consistently on the web. (0w)My increasingly youthful kinfolk mate has been averaging 20k all through continuous months and he works around 24 hours reliably. I can’t trust how direct it was once I attempted it out. This is my essential concern…:) GOOD LUCK
For more info visit………….. http://www.Smartcash1.com

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x