Dk Slaa avuliwa hadhi ya ubalozi

RAIS Samia Suluhu Hassan amemvua hadhi ya ubalozi Dk Wilbroad Slaa.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, iliyotolewa leo Septemba Mosi, 2023 imesema kuwa Dk Slaa amevuliwa hadhi hiyo kuanzia leo hii.

Dk Slaa aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Novemba 2017 na aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli.

Advertisement

Pia, alihidhinishwa kwa nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.

Kipindi Dk Slaa anateuliwa kuwa Balozi, alikuwa anaishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya siasa wa Ukawa.

2 comments

Comments are closed.