Dk Tulia Ackson mgeni rasmi siku ya mtoto wa kike duniani
DSM: SPIKA wa Bunge Dk.Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kuazimisha siku ya mtoto wa Kike duniani kesho Oktoba 11, 2023 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msichana Initiative, Rebecca Ng’umi amesema wameshirikiana na mashirika kama Flaviana Matata Foundation, Msichana Initiative, Sema na Tai storytelling for Social Change katika kusheherekea siku ya mtoto wa kike duniani.
“Tunatarajia kuwa na spika wa bunge la Tanzania Tulia Ackson aweze kuwasikiliza mabinti kilio chao tunaposema wapewe nafasi za kurudi shule wanapopata ujauzito na wakiwa tayari wamesha jifungua kupata nafasi ya kuendelea na masomo.
Amesema kuwa kampeni ya kumlinda mtoto wa kike walioiita Ajenda ya Msichana,
Kampeni hiyo inakwenda sambamba na kumpatia mtoto wa kike elimu katika kusheherekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike inayoadhimishwa Oktoba 11 ya kila mwaka ili kusherehekea mafanikio na uwezo wa msichana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya Elimu Faraja Nyarandu amesema kuwa thamani ya msichana inaanza na yeye kujithamini kisha wengine wanakuthamini.
“Tunaweza kutumia muda kuwapa elimu wasichana kujitambua na kujithamini ila utayari anakuwa nao yeye mwenyewe na sio mtu mwingine kwanza utayari yanayofata kutimiza ndoto zao.”amesema faraja