Dk Tulia alipongeza jeshi la polisi Mbeya

Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kuzuia na kupambana na uhalifu sambamba na ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kijamii.

Dk Tulia ametoa pongezi hizo leo wakati akikabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni seti nne ya jezi na mipira minne kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Dk Tulia ameahidi kuendelea kushirikiana na kuliunga mkono jeshi hilo katika kuendeleza michezo kwa kutoa vifaa vya michezo na kudhamini ligi na mashindano mbalimbali.

Advertisement

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amemshukuru Dk Tulia na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali hasa katika kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa wa huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *