Dk Tulia ateta na Polisi Wanawake

awataka kugombe anafasi za uongozi

DODOMA: Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson amewataka wanamtandao wa Polisi wanawake Tanzania (TPF-Net) kuchukua hatua na kuingia kwenye kamati, kugombea nafasi za juu zilizopo kwenye Jumuiya ya Polisi Wanawake wa Kimataifa (IAWP) hasa kipindi hiki ambacho uchapakazi wa  Samia Suluhu Hassan unafanya watanzania wenginewaweze kujulikana huko duniani.

Rai hiyo imetolewa leo Novemba 11, 2023 katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha matembezi maalum ya kumpongeza Spika kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-Net).

Dk Tulia alisema kuwa nafasi hii tumeipata sisi sote kama Taifa, pamoja na kwamba yeye ametangulia mbele, kazi yetu ni kuilinda hiyo nafasi kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri ili kutoa fursa kwa watanzania wengine watakaokuwa wanaenda kugombea huko watu waseme kuwa tunawajua watanzania huwa wanafanya vizuri na wana bidii, hivyo ameomba vyombo vingine vya ulinzi na usalama kushirikiana kwa pamoja katika kazi hiyo.

 

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF-Net), CP Suzan Kaganda kwa niaba ya Jeshi la Polisi naWanamtandao wa Polisi Wanawake Tanzania alimpongeza kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27, nchini Angola katika mkutano wa 147.

Kamishna Kaganda alisema kuwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa 31 umoja huo wa mabunge duniani akiwa kiongozi wa kwanza mwanamke kushika wadhifa huo kutoka Tanzania na bara la Afrika umewapa motisha na kuwahasisha askari wa kike na hakika ni heshima kubwa kwa nchi yetu na taifa kwa ujumla.

“Nafasi hii ni chachu kwa askari wa kike na wanamtandao kuhusu mtazamo na uwiano wa nafasi za kugombea katika kushika nafasi za juu za uogozi.” Alisema CP Kaganda.

Aidha, Kamishna Kaganda alikabidhi zawadi kwa Spika wa Bunge Dk.Tulia ambayo iliandaliwa na mtandao wa Polisi Wanawake ikiwa kama alama na kumbukumbu kwenye maisha yake baada ya kumaliza muda wake.

Matembezi hayo maalum yalihudhuriwa wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya Dodoma Mji, Polisi Kata wa Wilaya ya Dodoma pamoja na kikundi cha Jorging cha Ilazo yalianza katika viwanja vya Bunge na kuhitimishwa katika viwanja vya Nyerere Square.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
28 days ago

I get paid more than 90$ to 400$ per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily $10k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
.
.
.
Here is I started.…………>> http://remarkableincome09.blogspot.com

Julia
Julia
28 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month I have earned and received $18,539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online.
.
.
Detail Here——————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Joyceieves
Joyceieves
28 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 28 days ago by Joyceieves
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x