Dk Yonazi akutana na mwakilishi wa Vesterbacka

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi amekutana na mazungumzo na Mwanzilishi wa Kampuni ya Vesterbacka Finest Future na Mchezo wa Kompyuta (game) ujulikanao kama Angry Birds, Peter Vesterbacka jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijikita katika mikakati mbalimbali ya kuikuza sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, ikiwemo kubadilishana wataalamu ili kujifunza fursa mpya zitokanazo na sekta huyo.

Vesterbacka ni mjasiriamali kutoka nchini Finland.

Peter kwa sasa ni Profesa msaidizi wa Ubunifu na Ujasiriamali katika Chuo Kikuu cha Tongji kilichopo nchini China.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Tanzania, Dk Nkundwe Moses Mwasaga.

Habari Zifananazo

Back to top button