Dola milioni 332 kuimarisha GPE

RAIS mstaafu wa awamu ya nne,Dk Jakaya Kikwete amesema Taasisi ya ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) ni wadau muhimu katika maendeleo ya elimu nchini na kwamba kupitia wao jumla ya Dola milioni 332 zimetolewa kuimarisha sekta hiyo.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya GPE amesema hayo leo Dar es Salaam baada ya Ofisa Mtendaji wa Taasisi hiyo,Loura Frigenti kutembelea shule ya msingi ya Majimatitu iliyoko Mbagala na shule ya msingi ya Mikongeni iliyopo eneo la Gongolamboto.

Mbali na ziara hiyo, wajumbe wa Bodi ya GPE watafanya mkutano wiki ijayo Desemba 5 hadi 6,2023 ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkutano kama huo kufanyika nje ya bara la Ulaya.

Akizungumza Rais Kikwete amesema Taasisi hiyo imekuwa mshirika wa maendeleo kwa takriban miaka 13 na inafanya kazi ya kuboresha mazingira ya elimu kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Amesema GPE inatoa kipaumbele kwa elimu ya mtoto wa kike na kwamba kwa kipindi chote hicho jumla ya wanafunzi wenye mahitaji maalum 30,000 wamenufaika kwa kusaidiwa kusoma.

Amesema GPE imewezesha walimu takriban 43,000 kunufaika,ujenzi wa madarasa 400 nchini na mabweni 30,hayo yote ikiwa ni jitihada za kuboresha elimu nchini kuwa ya kiwango kinachostahili na asiwepo hata mmoja atakayeachwa bila elimu.

“GPE itaendelea kusaidia Tanzaniia, inajivunia kuona jinsi ambavyo fedha wanazozitoa zinavyotumika vizuri,” amesema Kikwete na kuongeza kuwa zipo nchi 82 duniani ambazo zinanufaika.

Ameongeza kuwa kupitia GPE kiwanda Cha kuchapisha na kusambaza vitabu vya kiada kilifufuliwa kwa gharama ya sh milioni 10, ambacho kiliwezesha wanafunzi kutodoroa kuelimisha hususani kipindi kile Cha mlipuko wa COVID 19.

Kuhusu shule alizotembelea amesema zinaridhisha katika kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayeachwa na Kwa shule ya Majimatitu madarasa nane na matundu ya vyoo sita yamejengwa chini ya mpango wa GPE na Kwa shule ya Mikongeni madarasa mawili na matundu

Kwa upande wa Frigenti, amesema lengo la GPE ni kuhakikisha hakuna atakayeachwa lakini pia mwanafunzi aweze kupata elimu iliyo bora na ya viwango.

Amesema kupitiai msaada inayotolewa uwiano wa mwanafunzi na Mwalimu utaimarishwa, uboreshaji wa madarasa lakini pia kuhakikisha madawati yanatosheleza wanafunzi.

Ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na kwamba serikali isisitenkuchukua hatua dhidi ya changamoto zinazomkabili shule Ili kuwa na elimu Bora yenye kutimiza mdoto za wanafunzi.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button