KAMPUNI ya Nigeria na nyingine kutoka nchini Ujerumani zimesaini mkataba wa Dola milioni 500 wa nishati mbadala na gesi.
Benki ya Muungano ya Nigeria na kundi la DWS la Ujerumani zimetiliana saini mkataba wa maelewano (MoU) kuhusu nishati mbadala unaolenga uwekezaji katika miradi ya nishati mbadala hasa maeneo ya vijijini.
Makubaliano ya pili kuhusu ushirikiano wa mauzo yalikubaliwa kati ya Riverside LNG ya Nigeria na Johannnes Schuetze Energy Import AG Ujerumani.
Aidha, chini ya mkataba huo, Nigeria itasambaza tani 850,000 za gesi asilia kwa Ujerumani kila mwaka ambayo inatarajia kuongezeka hadi Dola milioni 1.2 ambapo usafirishaji wa kwanza utakuwa 2026.