‘DP World haitakuwa na mamlaka kupunguza wafanyakazi’

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Hamza Johari, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Majadiliano kuhusu mwekezaji mpya kwenye bandari ya Dar es Salaam, amewaondoa hofu Watanzania juu ya mustakabali wa kazi zao mwekezaji mpya katika bandari ya  Dar es Salaam ataakapoanza kazi.

Johari amesema Kampuni ya DP World,  haitokuwa na mamlaka yoyote ya kuamua kupunguza wafanyakazi katika  bandari ya Dar es Salaam, kwani wafanyakazi hao watalindwa na Bunge la Tanzania.

“Bunge likiridhia hawezi kuja kusema akae sjui na TPA aseme sjui naona nipunguze hawa wafanyakazi haiwekezekani, maana bunge likisharidhia limelinda au limehakikisha.

“Ninaomba niwaondoe hofu, na ni lazima tuwe wazalendo vita zinazopigwa ni kubwa na ndio maana watu walioanza kuongea mwanzo kabisa ni taifa la jirani, ”amesema Johari.

Habari Zifananazo

Back to top button