Dr Dre kupewa tuzo

NGULI wa  muziki wa hip Hop nchini Marekani, Dr Dre anatarajia kupokea tuzo ya ‘ASCAP Hip Hop Icon’  kutokana na mchango wake mkubwa katika muziki huo, sherehe iliyopangwa kufanyika usiku wa leo mjini Los Angeles.

Dre ameweka msingi mkubwa katika muziki huo akiwainua wasanii mbalimbali kama 50 Cent na Eminem na anatambulika kwa namna alivyobadilisha utamaduni wa hip hop na ‘style’ yake ya ‘G Funk’.

Mwenyekiti wa Bodi na Rais wa ASCAP, Paul Williams amemzungumzia Dre kama mtu muhimu katika tasnia ya muziki wa hip hop na wanayo furaha kumpatia tuzo hiyo kama njia mojawapo ya kuutambua mchango wake.

Huu ni mwaka wa tuzo kwa msanii huyo ambapo mnamo mwezi Februari alitunukiwa tuzo ya Grammy kwa mchango wake katika hip hop inayokwenda kutimiza miaka 50 toka kuasisiwa kwake.

Habari Zifananazo

Back to top button