PRINCE Dube kutua Msimbazi? unaweza kuuliza hivyo mara baada ya klabu ya Azam FC kuthibitisha kupokea ofa kutoka Simba SC.
Awali kulikuwa na sintofahamu kuhusu uhamisho wa Dube baada ya kutangaza kuachana na timu hiyo.
Taarifa iliyotolewa usiku huu na klabu hiyo, imeeleza kuwa licha ya kupokea ofa hiyo, Al-Hilal ya Sudan pia imeonesha nia ya kumtaka.
Uongozi wa Azam umesema unazifanyia kazi ofa hizo, hata hivyo wamevikaribisha vilabu vingine kuweka ofa endapo vinamhitaji Mzimbabwe huyo.