Dulla Mbabe kulipa kisasi kesho?

ARUSHA; Mabondia, Abdallah Pazi maarufu Dulla Mbabe kutoka Tanzania na Erick Katompa kutoka DR Congo wamepima uzito tayari kwa pambano lao la siku ya kesho jijini Arusha.
Baada ya kupima uzito na kuthibitishwa kwa uwepo wa pambano hilo mabondia hao wametoa tambo kila mmoja akijinasibu kumlambisha sakafu mwenzake mapema kabisa kwenye pambano hilo.
Wakitoa tambo zao jijini Arusha kuelekea pambano hilo bondia Dulla Mbabe amesema taifa lipo kwenye mikono salama
 
” Kwanza niko salama na nawashukuru ndugu zetu Arusha na wote na niko tayari kwa pambano na nasema tena Katompa hawezi kutoka,”
 
Ameeleza watu wengi wamekuwa wakimsifia Katompa lakini hajaona uzuri wake na kuthibitisha hilo ameweza kupata matokeo chanya kwangu na ameyapata akiwa ametoka katika mechi ngumu hivyo hakuwa amepumzika safari hii ajiandae hatomuacha.
Kwa upande wake Katompa amesema amepata mazoezi yake ya kutosha tayari kumtandika mpinzani wake.
“Nitampiga Dulla Mbabe, Watanzania mje wengi mfike kushuhudia nitafanya kazi yangu ,” amesema Katompa.
 
Naye Juma Mwambelo Ofisa Mipango kampuni Lady in Red Promotion ambao ndio waandaaji amesema pambano hilo lina namna ya utofauti na mapambano yale ambayo watu wameyazoea.
 
“Hili ni la kisasi na mnajua mara ya mwisho Dulla Mbabe alipigwa na Katompa lakini leo ameudhihirishia umma wa Watanzania kuwa hawezi akapigwa tena,”amesema Mwambelo.
Pambano la wawili hao litatanguliwa na mapambano mengine saba yakihusisha mabondia wanawake na wanaume.
 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button