BUNGE la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), limepitisha muswada wa Kamisheni ya Huduma za Fedha ya Afrika Mashariki (EAC).
Muswada huo wa mwaka 2022 unalenga kuanzishwa kwa kamisheni kama taasisi huru yenye majukumu, mamlaka, vyanzo vya fedha na makao yake makuu.
Kupitishwa kwa muswada huo muhimu jana ni kuelekea utekelezaji wa Itifaki ya kuanzishwa kwa Umoja wa Fedha Afrika Mashariki.
Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo katika kikao cha nne cha Bunge kinachoendelea jijini Arusha, Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Bajeti, Denis Namala, alisema muswada huo umechelewa kwa zaidi ya miaka minne licha ya umuhimu wake tangu kukubaliwa kwa itifaki ya Umoja wa Fedha
Comments are closed.