JUMUIYA ya Uchumi ya Mataifa ya Magharibi mwa Afrika (*ECOWAS*) imelitaka taifa la Senegal kupanga upya tarehe ya uchaguzi wa rais.
ECOWAS imeeleza kuwa uamuzi wa kuahirisha uchaguzi hadi Desemba ni kinyume na katiba ya taifa hilo.
Hapo awali jumuiya hiyo ilisema kuahirishwa huko kulikwenda kinyume na utamaduni wa kidemokrasia wa Senegal, iliwataka wahusika wote katika mchakato wa uchaguzi kuzingatia uamuzi wa Baraza la Katiba.
Mapema leo, Msemaji wa Serikali, Abdou Karim Fofana alisema serikali ilizingatia uamuzi wa baraza hilo, lakini hakutaja kama hii inamaanisha kuwa ingeuzingatia.
Alisema pande tofauti za kisiasa zitahitaji kuzungumza na kila mmoja kutafuta njia ya kusonga mbele.