Ekari za mirungi zateketezwa Same  

EKARI 535 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa na watuhumiwa saba kukamatwa katika oparesheni maalum ya ‘Tokomeza Mirungi’, iliyoanza kutekelezwa ndani ya vijiji vinne katika Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

Katika oparesheni hiyo iliyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Usalama vijiji vilivyohusishwa ni Rikweni, Heikondi, Tae na Mahande.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa oparesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA ,Aretas Lyimo amesema ekari hizo zimeteketezwa kwa muda wa siku nane kuanzia Julai 2 hadi 9, mwaka huu.

“Tumeona hekari nyingi imetushangaza, hatukutegemea kuna hekari kubwa kiasi hiki hadi tunachukua vikosi vya Jeshi JKT kuja kufanya oparesheni hii na kununua mashine za kuteketeza kutokana na ukubwa wa hili eneo tutaendelea kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kilimo cha mirungi, ili waweze kuacha kilimo hiki na kwenda kulima kilimo mbadala,”ameeleza.

Habari Zifananazo

Back to top button