El Nino yaacha athari mikoa mitano

TANGA; Mvua za El Nino zimesababisha athari kubwa katika miundombinu ya barabara na madaraja katika Mikoa ya Dar Es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Songwe.

Akitoa tathimini hiyo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara TANROAD nchini, Mhandisi Mohamed Besta wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya  ukaguzi wa kalavati kwenye eneo la Bwiko barabara kuu ya Mombo Same.

Advertisement

Amesema kuwa mikoa hiyo imeleta athari kubwa kwa miundombinu ya barabara kuharibika,ikiwemo na madaraja kukatika hali ambayo imesababisha changamoto na athari kwa watumiaji wa barabara

“Mvua hii ambayo imenyesha kwa kiwango kikubwa imeleta athari lakini  kwa kiwango kikubwa tumeweza kukarabati maeneo mengi ambayo yalikosa mawasiliano na sasa yanapitika”amesema Mhandisi Besta

 

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *