Elimu ufundi stadi kuimarisha nguvu kazi

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa elimu ya ufundi stadi ni vema iimarishwe ili kutoa ujuzi kwaajili ya nguvu kazi inayohitajika katika sekta ya ajira.

Akifungua kongamano la siku mbili leo Jijini Arusha, lililoshirikisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi, Prof Joyce Ndalichako amesisitiza kuimarisha ujuzi unaohotajika katika soko la ajira.

Amesema elimu hiyo kuimarishwa zaidi ili kuwajengea uwezo vijana waweze kujiajiri sanjari na kuajiri wengine ili kuinua uchumi kwa vijana wanaohitaji kuonyesha uwezo wao katika bunifu mbalimbali pamoja na miradi

Advertisement

Naye Dk, Adolf Rutayuga ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)amesema kongamano hilo la siku mbili limehudhuriwa na wadau wa ndani na nje ya nchi na ndani lengo ni kuangalia jinsi ya kuinua ujuzi kwa vitendo unaendelezwa ili kuzalisha ajira au waweze kujiajiri.

Awali Msozi Nyirenda ambaye ni Kaimu Mkurugenzi na Utafutaji Rasilimali na Mitaji amesema suala la ajira nchini limekuwa ni changamoto kwa vijana hivyo wameamua kutoa mafunzo ili vijana waweze kuupata utakaowasaidia kubuni mbinu mbalimbali za kibiashara ikiwemo sekta ya ajira

“Vijana zaidi ya 48000 wanefadhiliwa kwa kupewa mafunzo ili waweze kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa ”

Wakati huo huo,Profesa Eddatandi Luoga ambaye ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anasisitiza mafunzo kwavitendo yanazalisha watanzania kujifunza mbinu mbalimbali katika sekta ya biashara.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *