Elirehema :msije BOT fuateni taratibu

BENKI Kuu ya Tanzania ‘BOT’ kupitia Mhasibu Mwandamizi Mkuu wa Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Elirehema Msemembo amesema mteja yeyote anayesubiri stahiki za malipo ya mirathi asisumbuke kufika BOT hata ikiwa akaunti yake ipo hapo.

Kauli hiyo imetolewa leo katika banda la BOT lililopo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea ndani ya viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, wilayani Temeke, Dar es Salaam.

“Mteja mmoja mmoja anaguswa na huduma zetu pale anapofanya malipo kwenda serikalini au anapo pokea malipo kutoka serikalini.” Amesema

Aidha, amesema kwa yule anayesubiri malipo ya mirathi hapaswi kusumbuka kwenda BOT badala yake atapaswa kufuata taratibu zinazowekwa kutoka mahakamani na atapokea stahiki zake kupitia benki husika.

Habari Zifananazo

Back to top button