Elneny asaini mkataba mpya Arsenal
Kiungo wa Arsenal, Mohamed Elneny amesaini kataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Mmisri huyo ndiye mchezaji aliyekaa muda mrefu zaidi kwenye klabu hiyo.
Mo ambaye alijiunga Arsenal mwaka 2016 akitokea Basel ya Uswisi ataendelea kuwatumikia washika bunduki wa London hadi Juni 2024.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri ameichezea Arsenal mechi 155 katika mashindano yote, akifunga mabao sita na kusaidia mara 10 katika miaka saba aliyoitumikia klabu hiyo.
“Nina furaha sana, ninaipenda klabu hii na wafuasi wetu sana na nitatoa kila kitu kuhakikisha tunakuwa bora zaidi tuwezavyo, kila siku niko hapa,” kiungo huyo amesema.