England yafuzu Euro, Italia Ukraine mchujo
KIKOSI cha England kilihitaji pointi moja kufuzu michuano ya Euro, lakini ilionekana kama sherehe zao zingechelewa au kutokuwepo baada ya mshambuliaji wa zamani wa West Ham United, Gianluca Scamacca kuipa Italia bao la kuongoza dakika ya 15.
–
Mshambuliaji wa Bayern Munchen, Harry Kane alirejesha matumaini baada ya kufunga penalty dakika ya 35 na kufikisha mabao 60 akiwa na timu hiyo na mchezo huo kwenda mapumziko ubao ukisomeka 1-1.
–
Marcus Rashford aliifungia England bao la pili dakika ya 57 kabla ya Kane kuzima matumaini ya Italia alipofunga bao la tatu kwa zikiwa zimesalia dakika 13, mchezo kumalizika.
–
Ushindi huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Uingereza nyumbani dhidi ya Italia tangu Novemba 1977 na kukamilisha ushindi wa mara mbili katika kundi baada ya ushindi huko Naples mnamo Machi.
–
England wamo kileleni mwa Kundi C wakiwa na pointi 16, huku kichapo hicho kinamaanisha Italia wapo nafasi ya tatu na watacheza na Ukraine katika mechi yao ya mwisho ya mchujo katika mechi ambayo itakuwa ya kuamua nani atashika nafasi ya pili.