BREAKING: Kocha Luis Enrique ameachana na timu ya Taifa ya Hispania, ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kutolewa na Morocco katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea Qatar. Shirikisho la Soka Hispania ( RFEF) limethibitisha.
Kocha wa timu ya vijana 21, Luis De la Fuente ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo, akichukuwa nafasi ya Enrique.
RFEF ilitoa taarifa ya kumshukuru Enrique kwa huduma yake na kueleza nia yake ya kuanzisha mradi mpya wa timu ya taifa.
Taarifa hiyo ilithibitisha kuwa mkataba wa Enrique unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu hautaongezwa tena.
Uhispania ilishindwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano hiyo iliyofanyika Qatar baada ya kushindwa na Morocco kwa mikwaju ya penalti siku ya Jumanne.
Enrique alisema baada ya mechi hiyo kuwa yeye ndiye wa kulaumiwa kwa kushindwa.
kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa akiiongoza Uhispania tangu 2018, na sasa kuna uwezekano wa kurudi kufundisha timu za klabu.