EPL kuendelea leo

Michezo mbalimbali ya Ligi Kuu nchini England ‘EPL’ inaendelea leo ambapo Arsenal itakuwa katika Uwanja wa King Power wakialikwa na Leicester City mchezo ambao utapigwa saa 12:00 jioni.

Mchezo mwingine utakaopigwa muda huo ni Everton dhidi ya Aston Villa, Leeds watakuwa nyumbani kuwaalika Soton, wagonga nyundo wa London ‘Westham United’ watakuwa nyumbani kuwaalika wakata miti ‘Notts Forest’.

Mchezo mwingine Manchester City watakuwa Uwanja wa Vitality wakialikwa na Bournemouth mchezo utakaopigwa saa 2:30 usiku.

Mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Crystal Palace dhidi ya Liverpool, mechi hiyo itapigwa saa 4:45 usiku.
Kesho pia ligi hiyo itaendelea ambapo Chelsea itakuwa nyumbani Stanford Bridge wakiwaalika Spurs ya Conte.

Habari Zifananazo

Back to top button