EPL kusimama wiki tatu

BAADA ya raundi ya 28 Ligi Kuu England (EPL) wikiendi hii, ligi hiyo sasa itasimama kwa wiki tatu kupisha michezo ya Kombe la FA na mechi za mataifa.

EPL itarejea Machi 30, ambapo vinara Arsenal watakuwa Etihad kuvaana na Manchester City, na Liverpool watakuwa Anfield kuwaalika Brighton & Hove Albion.

Ligi hiyo inaenda mapumziko Arsenal akiongoza kwa pointi 64 sawa na Liverpool tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.

Manchester City wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 63, baada ya leo kukamilisha raundi ya 28.

Kabla ya kwenda mapumzikoni, leo Jumatatu saa 5 usiku kutakuwa na mchezo mmoja wa EPL kati ya Chelsea na Newcastle United.

Habari Zifananazo

Back to top button