RAUNDI ya 26 Ligi Kuu England inaendelea leo na kesho, ambapo mchezo wa mapema zaidi utakuwa kati ya Manchester City dhidi ya Newcastle United, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Etihad saa 9:30 mchana.
Arsenal itakuwa nyumbani Emirates kuwakaribisha Bournemouth, Chelsea watakipiga dhidi ya Leeds, Aston Villa itakuwa Villa Park kukipiga na Crystal Palace, Brighton na West Ham United, Wolver na Spurs, michezo yote itapigwa saa 12:00 jioni.
Mchezo wa mwisho kwa leo utakuwa katika Uwanja wa St Marry wakati Soton itakapoialika Lecister City, mchezo huo utapigwa saa 2:30 usiku.
Kesho ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Liverpool itakuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester United, na Notts dhidi ya Everton. Jumatatu kutakuwa na mchezo mmoja Brentford dhidi ya Fulham.